Home » Afrika » Kifaa maalum kinachotumika kuripoti visa

Kifaa maalum kinachotumika kuripoti visa

04 February 2016 | Afrika

Visa vya dhuluma za kijinsia dhidi ya watoto vimekuwa vikiripotiwa mara kwa mara hasa katika eneo la Pwani ya Kenya, vikidaiwa kuchangiwa na mila za jadi na jamii kutoripoti visa hivyo kwa idara husika, kwa hofu ya unyanyapaa.

 

Shirika moja la kimataifa linalofadhili miradi ya kijamii kuhudumia watoto la Plan international katika jimbo la Kilifi huko Pwani nchini Kenya, limezundua kifaa maalum kinachotumika kuripoti visa hivyo kwa idara husika kupitia simu yenye mtandao wa internate.

Ad