Home » Afrika » Kenya kujenga jela mpya ya kuwazuia wafungwa wenye itikadi kali.

Kenya kujenga jela mpya ya kuwazuia wafungwa wenye itikadi kali.

17 February 2016 | Afrika

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema Kenya itajenga jela mpya ya kuwazuia wafungwa wenye itikadi kali.

Katika hotuba yake wakati wa hafla ya kufuzu kwa zaidi ya askari jela 2,000 hapo jana raisi Kenyata alisema hatua hiyo imelenga kuzuia wafungwa hao kutoeneza itikadi hizo kwa wafungwa wengine.

Kwa sasa ni wafungwa waliohukumiwa kunyongwa pekee ambao hutengwa na wafungwa wengine gerezani.

Askari jela pia wamelalamikia hali duni ya mazingira ya kufanyia kazi pamoja na malipo duni ambavyo raisi ameahidi kuyashughulikia.

Ad