Home » Afrika » Jumuiya ya kimataifa inaelekea kukosa uvumilivu

Jumuiya ya kimataifa inaelekea kukosa uvumilivu

25 March 2016 | Afrika

Viongozi wanaosimamia zoezi la usitishwaji mapigano nchini Sudani Kusini wamevionya vikosi vya pande mbili zinazokinzana nchini humo kuwa jumuiya ya kimataifa inaelekea kukosa uvumilivu kufuatia hatua yao ya kushindwa kutekeleza mkataba wa amani walioutia saini miezi 7 iliyopita.

Mkuu wa ujumbe unaosimamia utekelezwaji wa makubaliano ya amani, rais wa zamani wa Botswana, Festus Mogae, amesema timu yake itahakikisha mkataba huo wa amani uliotiswa saini mwezi August mwaka jana unatekelezwa licha ya mapigano kuendelea kushudiwa.

Rais Mogae, amezionya pande hizo na kuongeza kuwa kutotekeleza mkataba wa amani walioutia saini ni kuijaribu jumuiya ya kimataifa na kwamba uvumilivu wake unaelekea kufikia mwisho.

Ad