Home » Afrika » Huko nchini Kenya mcheza kamari raia wa Tanzania ameuawa

Huko nchini Kenya mcheza kamari raia wa Tanzania ameuawa

09 February 2016 | Afrika

Huko nchini Kenya mcheza kamari raia wa Tanzania ameuawa na kundi la watu kwa kupigwa mawe,baada ya kuwaua watu wawili kufuatia kupoteza pesa zake katika mchezo huo na kushindwa kukubaliana na hali hiyo, polisi wamesema leo Jumanne.

Mtanzania huyo  alipandwa na  hasira baada ya kupoteza dola 300 katika casino moja wilayani  Eastleigh mjini Nairobi  majira ya asubuhi leo  Jumanne, na kumshambulia meneja wa casino baada ya kukataa kumkopesha fedha ili aendelee kucheza.

Kwa mujibu wa mkuu wa polisi jijini Nairobi Japhet Koome,mtu huyo baada ya kunyimwa pesa  aliondoka na kurejea na  panga na kumshambulia meneja huyo mwanamke na kumwua kisha akamvamia mlinzi ambaye alijaribu kuingilia na kumua pia kabla ya kukamatwa na wacheza kamari wenzie na kumwua kwa kupiga mawe

Ad