Home » Afrika » Cameroon vimetekeleza mashambulizi Boko Haram nchini Nigeria,

Cameroon vimetekeleza mashambulizi Boko Haram nchini Nigeria,

17 February 2016 | Afrika

Vikosi vya Serikali ya Cameroon vimetekeleza mashambulizi kulenga kambi muhimu za wapiganaji wa kundi la Boko Haram nchini Nigeria, huku ikiripotiwa kuuawa kwa wapiganaji wengi wa kundi hilo pamoja na kukamata zana za kivita zilizokuwa zinatumiwa na wapiganaji hao.

 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na jeshi la Cameroon imesema kuwa operesheni dhidi ya wapiganaji wa Boko Haram, ilitekelezwa juma moja lililopita kwenye eneo la Ngoshe, eneo la mpaka wa nchi hiyo na Nigeria.

 

Msemaji wa jeshi la Cameroon, Issa Tchiroma Bakary, amethibitisha kutekelezwa kwa operesheni hiyo na kuongeza kuwa, wapiganaji 162 wa Boko Haram waliuawa, huku mateka zaidi ya 100 wakiokolewa wakiwemo raia 15 wa Cameroon.

Ad