Michezo
14 January 2016
Klabu ya soka ya URA ndio mabingwa wa taji la Mapinduzi Visiwani Zanzibar mwaka 2016.
URA iliishinda Mtibwa Sugar kutoka Tanzania bara kwa kuifunga mabao 3 kwa 1 katika fainali iliyochezwa Jumatano usiku katika uwanja wa Amman Visiwani Zanzibar.
Julius Ntambi alikuwa wa kwanza kuipa URA bao la ufunguzi katika kipindi cha kwanza cha mchuano huo,... [Read More]
14 January 2016
Rwanda inaingia katika vitabu vya kihistoria kwa kuandaa mashindano makubwa ya soka barani Afrika kwa wachezaji wanaocheza nyumbani CHAN, kuanzia Jumamosi hii.
Hii ni mara ya kwanza kwa mashindano haya kufanyika nchini Rwanda na katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kat,i tangu kuzinduliwa kwake mwaka 2009 nchini Cote D'voire.
Serikali ya Rwanda... [Read More]
12 January 2016
Hatua ya Lionel Messi kunyakua taji la mchezaji bora katika mchezo wa soka duniani kwa mara ya tano na kuweka historia ya kuwa mchezaji wa kwanza kuwahi kufikia kiwango hicho, inaweka wazi mafanikio ya mshambuliaji huyu matata.
Messi mwenye umri wa miaka 28 raia wa Argentina, alianza kuichezea Barcelona mwaka 2001 akiwa kijana chipukizi na hadi... [Read More]
12 January 2016
Timu ya taifa ya soka ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inayowajumuisha wachezaji wanaocheza soka nyumbani, Itaanza kuwani ubingwa wa michuano ya Afrika CHAN, dhidi ya Ethiopia siku ya Jumapili katika uwanja wa Huye mjini Butare.
Leopard imeshiriki katika makala yote ya CHAN tangu kuanzishwa kwake mwaka 2009 nchini Cote D'voire, mwaka ambao... [Read More]
09 January 2016
Michuano ya soka ya CHAN kuwania ubingwa wa Afrika baina ya wachezaji wanaocheza soka nyumbani, intarajiwa kuanza Jumamosi ijayo tarehe 16 mwezi huu nchini Rwanda.
Mataifa 15 pamoja na Rwanda yatashiriki katika michuani hii inayitarajiwa kuwakusanya maelfu ya wapenzi wa soka katika nchi hiyo ya Afrika ya Kati.
Serikali ya Rwanda imetangaza kuwa... [Read More]
08 January 2016
Nahodha wa timu ya taifa ya soka ya Cote D'voire na klabu ya Manchester City nchini Uingereza Yaya Toure amesema amesikitishwa sana kwa kukosa kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa soka barani Afrika mwaka 2015.
Toure mwenye umri wa miaka 32, alishinda taji hilo mara nne mfulilizo mwaka 2011, 2012, 2013 na 2014.
Toure ameongeza kuwa kutokana na juhudi... [Read More]
08 January 2016
Patrice Carteron ameondoka katika klabu ya soka ya TP Mazembe baada ya mkataba wake wa kuwa kocha kumalizika mwezi Desemba mwaka jana.
Uongozi wa klabu hiyo umetangaza rasmi kuwa umeachana na Carteron raia wa Ufaransa ambaye alijiunga na klabu hiyo yenye makao yake mjini Lubumbashi mwaka 2013 akitokea timu ya taifa ya Mali.
Kocha huyo atakumbukwa... [Read More]
08 January 2016
Bakary Papa Gassama kutoka nchini Gambia, kwa mwaka wa pili mfululizo ameshinda tuzo ya refarii bora barani Afrika.
Gassama mwenye umri wa miaka 36 alikuwa refarii wa FIFA mwaka 2007 na mwaka 2012 alikuwa miongoni mwa marefarii walioshiriki katika michuano ya Olimpiki na hasa fainali kati ya Mexico na Brazil lakini kipindi hicho alikuwa afisa... [Read More]
08 January 2016
Pierre-Emerick Aubameyang mshambuliaji wa timu ya taifa ya soka ya Gabon na klabu ya Borrussia Dortmund ya Ujerumani, ndio mchezaji bora wa mwaka 2015.
Aubameyang mwenye umri wa miaka 26 alipewa tuzo hiyo jijini Abuja jana usiku baada ya kupata alama 143 mbele ya mshambuliaji wa Manchester City na Cote Dvoire Yaya Toure aliyepata alama 136.
Andre... [Read More]
Pages
- « first
- ‹ previous
- 1
- 2
- 3