Home » Michezo » URA yashinda taji la Mapinduzi

URA yashinda taji la Mapinduzi

14 January 2016 | Michezo

Klabu ya soka ya URA ndio mabingwa wa taji la Mapinduzi Visiwani Zanzibar mwaka 2016.

URA iliishinda Mtibwa Sugar kutoka Tanzania bara kwa kuifunga mabao 3 kwa 1 katika fainali iliyochezwa Jumatano usiku katika uwanja wa Amman Visiwani Zanzibar.

Julius Ntambi alikuwa wa kwanza kuipa URA bao la ufunguzi katika kipindi cha kwanza cha mchuano huo, huku Peter Lwasa akifunga mabao mawili kipindi cha pili.

Bao la Mtibwa Sugar kuwafuta machozi lilitiwa kimyani na Jaffar Salum katika mchuano huo ambao Waganda waliutawala.

Peter Lwasa aliipatia klabu yake mabao 3 katika michuano hiyo huku Godfrey Villa Oromchan akifunga mabao mawili.

Taji la mwaka wa 2014 pia lilikwenda nchini Uganda na lilinyakuliwa na KCCA F.C ambayo ilishindwa kufika Zanzibar kutetea taji hili.

Michuano hii huchezwa kila mwaka kuadhimisha sherehe za mapinduzi ya Zanzibar ambayo hufanyika kila tarehe 12 mwezi wa Januari.

Orodha ya washindi wa taji la Mapinduzi.

2007 Yanga SC
2008 Simba SC
2009 Miembeni
2010 Mtibwa Sugar
2011 Simba SC
2012 Azam FC
2013 Azam FC
2014 KCCA
2015 Simba SC
2006 URA 

Ad