Home » Tanzania » Ni akina nani wanawake wengine kwenye Baraza la Mawaziri la Rais Samia?

Ni akina nani wanawake wengine kwenye Baraza la Mawaziri la Rais Samia?

02 April 2021 | Tanzania

Mheshimiwa Liberata Mulamula

Mheshimiwa Liberata Mulamula Waziri wa Mambo ya Nje 

 

Balozi Mulamula amezaliwa pacha na mwenzake na jambo moja ambalo rafiki zake wanalijua kuhusu mtumishi huyu ni mapenzi yake kwa senene -chakula maarufu kwa watu wa mkoa anaotoka wa Kagera.

 

 
Jenista Mhagama

CHANZO CHA PICHA,BUNGE /TZ

 

Jenista Mhagama (Ofisi ya Waziri Mkuu - Bunge, Vijana, Walemavu),

Kuondoa Mulamula, wanawake wengine katika baraza la mawaziri ni Jenista Mhagama (Ofisi ya Waziri Mkuu - Bunge, Vijana, Walemavu), Profesa Joyce Ndalichako (Elimu), Ummy Mwalimu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa -Tamisemi) na Dk. Dorothy Gwajima (Afya).

Jenista ni mwalimu kitaaluma lakini sasa anachukuliwa kama mmoja wa wanasiasa waandamizi wanawake hapa nchini.

Hiki ni kipindi chake cha nne bungeni na ingawa amekuwa machoni kwa umma kwa muda wa takribani miaka 20 sasa, si mwanasiasa mashuhuri ingawa kipaji chake kinaelezwa kuwa ndani ya siasa za Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Profesa Ndalichako ni msomi wa kiwango cha Shahada ya Uzamivu (PhD) na mwalimu kitaaluma na hana muda mrefu sana katika siasa - hiki kikiwa ni kipindi chake cha pili bungeni; akiingia kwa mara ya kwanza kwa kuteuliwa na Rais Magufuli.

 
Ummy Mwalimu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa -Tamisemi)
Ummy Mwalimu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa -Tamisemi)

Ummy Mwalimu ni mwanasiasa mwanamke ambaye heshima na nyota yake inaonekana kupaa kwa kasi.

Anatajwa kama mmoja wa wanasiasa wanaopendwa na Samia - yeye mwenyewe akizunguka naye katika maeneo mengi kumwombea kura wakati akiwania Umakamu wa Rais kwa mara ya kwanza mwaka 2015.

Gwajima ni daktari wa binadamu, akiwa amesomea taaluma hiyo Ulaya Mashariki na hii ndiyo mara yake ya kwanza kuwa mbunge kwa kuteuliwa kwake na Magufuli pia.

 
Dk. Dorothy Gwajima (Afya)
Dk. Dorothy Gwajima (Afya)

Kurejeshwa kwake katika nafasi hiyo na Samia kumewashangaza wakosoaji wake wengi ambao hawakufurahishwa na namna anavyopambana na janga la ugonjwa wa Corona.

Katika mabadiliko ya mawaziri yaliyofanywa na Rais Samia wiki hii, hakuna aliyeondolewa katika baraza na badala yake kuna waliohamishwa kutoka wizara moja kwenda nyingine.

Inaonekana Gwajima amepewa nafasi nyingine ya kuonyesha uwezo wake na Samia - kama ilivyokuwa kwa wengine na muda utaeleza namna gani atabadilika katika utawala mpya.

/BBC
Ad