#000000">MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania SAMIA SULUHU HASSAN ameitakaTaasisi ya Hans Seidel Foundation isaidie kupeleka elimu ya uraia bungeni ili wabunge wajue wajibu wao ndani na nje ya Bunge.
#000000">Mheshimiwa Samia Suluhu amekukutana na ujumbe wa Taasisi ya Hans Seidel Foundation uliomtembelea ofisi kwake Ikulu, Jijini Dar es salaam kutaka kujua kama ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuna sheria na kanuni za kuendesha vikao vya Bunge.
#000000">Makamu wa Rais aliueleza ujumbe huo ulioongozwa na Mwenyekiti wa Hans Seidel Foundation Prof. URSULA MANNK kuwa sheria na kanuni zipo za kuendesha vikao vya Bunge lakini baadhi ya wabunge hawazifuati kama inavyotakiwa.
#000000">Alisema Elimu ya uraia itasaidia katika kuwafanya wabunge hao wajenge nidhamu katika michango na ushiriki wao kwa ujumla ndani na nje ya Bunge.
Taasisi ya Hans Seidel Foundation yenye makao yake makuu Munich, nchini Ujerumani ambayo inajishughulisha na masuala ya demokrasia, amani na maendeleo huku ikitoa kipaumbele kwenye elimu ya uraia inaendesha shughuli zake katika nchi zaidi ya 60 duniani. Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais Dar es salaam.