UWASILISHWAJI WA MUSWADA WA SHERIA YA RELI YA MWAKA 2017 (THE RAILWAY ACT, 2017)
#Muswada unapendekeza kutungwa kwa sheria itakayoanzisha Shirika la Reli Tanzania (TRC) ambalo litakuwa na jukumu la kusimamia, kuendeleza miundombinu ya reli na kutoa huduma ya usafiri wa reli - Prof. Makame Mbarawa.
#Madhumuni ya muswada ni kuweka mfumo madhubuti wa utoaji huduma ya usafiri wa reli, usimamizi na uendelezaji wa miundombinu ya reli - Prof. Mbarawa.
#Muswada umezingatia vyanzo vya mapato ambavyo ni pamoja na mfuko wa reli, ruzuku toka Serikalini, nauli za abiria pamoja na tozo za usafirishaji wa mizigo - Prof. Mbarawa.
#Muswada umezingatia kuainisha utaratibu wa kutoa huduma ya usafirishaji wa abiria na mizigo - Prof. Makame Mbarawa.
#Kuainisha utaratibu wa kuratibu ujenzi na uendelezaji wa miundombinu ya reli ikiwa ni pamoja na uhifadhi wa eneo la reli - Prof. Makame Mbarawa.
Muswada unaainisha utaratibu wa kuhamisha watumishi kutoka TRL na RAHCO kwenda Shirika jipya - Prof. Makame Mbarawa.
MAONI NA USHAURI WA KAMATI YA BUNGE YA MIUNDO MBINU.
#Shirika Jipya liisaidie Serikali katika kufanya utafiti wa kupanua matawi ya reli ya kati kutoka Bandari kavu ya Isaka ( Shinyanga) hadi Rusumo Mkoani Kagera - M'Mwenyekiti Mhe. Moshi Kakosa.
#Ubomoaji au uondilewaji wa wananchi waliomo kwenye maeneo ya Shirika la reli uendelee isipokuwa, wananchi waliomilikishwa maeneo ya Shirika la Reli - M'Mwenyekiti Mhe. Moshi Kakosa.
MICHANGO YA WAHESHIMIWA WABUNGE
# Mpanda ina wasafiri wengi wanaotumia reli hivyo mabehewa yaongezwe - Mhe. Anna Lupembe.
#Kuwepo na kipengele kitakachoonyesha Shirika hilo jipya linatakiwa kutengeneza faida - Mhe. Hussein Bashe.
#Bodi iundwe na angalau mtu mmoja kutoka sekta binafsi kwani shirika litakuwa linatoa huduma kwa sekta binafsi pia - Mhe. Hussein Bashe.
#Tatizo la uchache wa mabehewa limesababisha wananchi wengi kushindwa kutumia usafiri huo - Mhe. Magdalena Sakaya.
Imeandaliwa na Idara ya Habari - MAELEZO.