Home » Tanzania » Usalama Barabarani kanda maalum ya Dar es salaam wa kusanya shilingi BILIONI (1.9)

Usalama Barabarani kanda maalum ya Dar es salaam wa kusanya shilingi BILIONI (1.9)

24 February 2016 | Tanzania

Kikosi cha usalama barabarani kanda maalum ya Dar es salaam kimetangaza kukusanya kiasi cha shilingi BILIONI MOJA NUKTA TISA (1.9) kutokana na faini za ukamataji wa makosa ya usalama barabarani kuanzia siku ya kwanza ya February 2016 mpaka tarehe 22 ya mwezi huu.

Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es salaam Simon Sirro amesema ‘Sio kwamba tunafurahia watu wafanye makosa ili tuingize pesa, hatupendi tuwe na pesa nyingi za makusanyo kwa ajili ya kuonea Wananchi… hapana, tunafanya hivyo kudhibiti na kuhakikisha kunakuwa na utii wa sheria‘

HIZO BILIONI 1.9 ZIMETOKANA NA HII ORODHA HAPA CHINI

  1. IDADI YA PIKIPIKI ZILIZOKAMATWA 4046
  2. IDADI YA MAGARI YALIYOKAMATWA 32528
  3. DALADALA ZILIZOKAMATWA 23,264
  4. MAGARI MENGINE (BINAFSI NA MALORI) 9264
  5. JUMLA YA MAKOSA YALIYOKAMTWA 36,574

Hii taarifa imekuja siku moja baada ya Wizara ya fedha kutangaza jana kukusanya mapato ya serikali na kufikia zaidi ya TRILIONI MOJA kwa mwezi February 2016 pekee ambao bado haujamalizika kikiwa ni kiwango tofauti na mwaka uliopita ambapo walikua wakikusanya kwenye BILIONI 800 n.k

Ad