UNESCO yafanya kongamano kujadili mpango wa maendeleo sekta ya Elimu
Katika kuhakikisha elimu ya Tanzania inakua yenye ubora zaidi, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limepanga kuisaidia Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi kuandaa Mpango wa Maendeleo katika Sekta ya Elimu (ESDP), mpango ambao umelenga kusaidia serikali ya Tanzania kutengeneza maudhui na mikakati ya kuendeleza elimu kwa upande wa Tanzania bara.
#000000">Akizungumzia mpango huo katika kongamano la siku mbili la kutambua vipaumbele vinavyotakiwa katika kuandaa mpango huo wa elimu, kwa niaba ya Kamishna wa Elimu wa Wizara ya Elimu, Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima na Elimu iliyo nje ya Mfumo rasmi kutoka Wizara ya Elimu, Salum Mnjagila alisema mpango huo unatarajiwa kufanya kazi kwa kipindi cha miaka mitano kwa kuanzia mwaka 2017 – 2021 ili kuona ni jinsi gani utabadili elimu ya Tanzania.
#000000">Alisema kupitia kongamano hilo wanataraji kuchagua baadhi ya vipaumbele ambavyo wataona vinaumuhimu zaidi kuanza navyo kwa miaka mitano ya kwanza kwa mpango huo na baadae wataanza utekelezaji wa vipaumbele ambavyo vitakuwa vimepewa kipaumbele na washiriki wa kongamano hilo.
#000000">“Tupo hapa kufanya tathimini ya vipaumbele ambavyo vimeletwa mbele yetu ili tufanyie uchambuzi na tuone ni vipaumbele vipi tutaviweka kwenye mpango wa miaka mitano katika kuboresha sekta ya elimu nchini,” alisema Mnjagila.
#000000">Nae Mkurugenzi Msaidizi wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Wizara ya Elimu, Makuru Petro ambaye ameshiriki kufanya uchambuzi wa elimu ya Tanzania kwa kushirikiana na wataalamu kutoka UNESCO alisema katika kuchambua elimu ya Tanzania wamegundua kuwa elimu imekuwa ikishuka na hilo linatokana na kuongezeka kwa wanafunzi wanaosajiliwa kuanza shule huku kukiwa hakuna maboresho ambayo yanafanyika ili kuboresha elimu hiyo.
#000000">Alisema baada ya uchambuzi kufanyika wanafanya tathmini ili kupata matokeo ambayo watajadili kwa pamoja kwa kushirikisha wadau mbalimbali kutoka mashirika ya kiserikali na yasiyo ya serikali ili kupitisha vipaumbele ambavyo vitafanyiwa kazi kati ya vipaumbele ambavyo wao waliwasilisha kwa washiriki hao.
#000000">“Elimu ya Tanzania hali sio nzuri tumefanya uchambuzi hata mashuleni hakuna hali nzuri mfano hata Geita tumekuta darasa moja linatumiwa na wanafunzi 80 hadi 100 na hilo ni tatizo na baada ya kuchambua changamoto na kuzifanyia tathmini tunazileta hapa ili tuchague vipaumbele vya kuanza kuvifanyia kazi,” alisema Petro.
#000000">Nalo Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kupitia kwa Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa shirika hilo nchini, Zulmira Rodrigues alisema lengo la kuweka mpango huo ni kuboresha elimu ya Tanzania kwa kuifanya kuwa bora na iliyo na usawa kwa makundi yote ya jamii kwa matokeo mazuri ya baadae.
#000000">Alisema kuna mambo ambayo yanatakiwa kupewa vipaumbele ikiwepo ni pamoja na ubora wa elimu, fursa za elimu kwa makundi yote katika jamii na kujenga uwezo kwa watendaji ambao wanatoa hiyo elimu kama ni walimu basi wawe wanapewa mafunzo kuendana na wakati uliopo ili kuwa na kitu kipya ambacho kinahitajika kwa wanafunzi kwa wakati huo.