Rais Magufuli ahutubia umati uliofanyika Musoma mjini katika viwanja vya Mukendo
06 September 2018 | Tanzania
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia wananchi
wa Musoma waliokusanyika katika viwanja vya Mukendo vilivyopo Musoma mjini kwa ajili ya
kumsikiliza mara baada ya kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Mara.
Sehemu ya wananchi waliohudhuria mkutano huo uliofanyika Musoma mjini katika viwanja
vya Mukendo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia dawati
ambalo alikuwa akilitumia kujisomea Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
katika Shule ya Msingi Mwisenge Musoma. Hayati Mwalimu Nyerere alisoma shule hapo
elimu ya Msingi tarehe 20/4/ 1934 hadi 1/10/1936.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na
Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa, mwakilishi wa Shirika la Maendeleo
la Ufaransa AFD Stephanie Mouen wakanza kulia mwenye wakivuta utepe
kuashiria ufunguzi wa mradi wa maji safi na usafi wa mazingira katika
manispaa ya Musoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akiwa pamoja na Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa
wakisikiliza maelezo ya mradi wa wa maji safi na usafi wa mazingira
katika manispaa ya Musoma mjini Mkoani Mara kabla ya kuuzindua.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Stephanie
Mouen mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa AFD Agence Francaise De Development
waliosaidia katika mradi huo wa maji Musoma mkoani Mara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akivuta utepe pamoja na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano
Mhandisi Isaack Kamwelwe wakivuta utepe kuashiria ufunguzi wa
barabara ya kutoka Mpakani mwa Simiyu/Mara na Musoma km 85.5.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Waziri
wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaack Kamwelwe mara baada ya kufungua
barabara ya kutoka Mpakani mwa Simiyu/Mara na Musoma km 85.5.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na
wananchi wa Musoma mjini (hawaonekani pichani) katika viwanja vya Mukendo Musoma
mkoani Mara. Picha namba 16. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli akitoka katika bweni alilokuwa akilala Baba wa Taifa Hayati
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika Shule ya Msingi Mwisenge Musoma.
Hayati Mwalimu Nyerere alisoma shule hapo elimu ya Msingi kuanzia
tarehe 20/4/ 1934 hadi 1/10/193. PICHA NA IKULU