MAKAMU WA RAIS APOKEA TAARIFA YA KIKOSI KAZI KUTOKA MBEYA
14 June 2017 | Tanzania
MAKAMU WA RAIS APOKEA TAARIFA YA KIKOSI KAZI KUTOKA MBEYA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea taarifa kutoka kwa Mkuu wa mkoa wa Mbeya Ndugu Amos Makala ya kikosi kazi cha mkoa wa Mbeya kuhusu mapendekezo ya marekebisho ya mpaka kati ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha na Vijiji kati ya Wilaya ya Mbarali na Chunya (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Mbeya Ndugu Amos Makala wakati wa uwasilishwaji wa taarifa ya kikosi kazi cha mkoa wa Mbeya kuhusu mapendekezo ya marekebisho ya mpaka kati ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha na Vijiji kati ya Wilaya ya Mbarali na Chunya (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza mbele Mkuu wa mkoa wa Mbeya Ndugu Amos Makala pamoja na kikosi kazi chake wakati wa uwasilishwaji wa taarifa ya kikosi kazi cha mkoa wa Mbeya kuhusu mapendekezo ya marekebisho ya mpaka kati ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha na Vijiji kati ya Wilaya ya Mbarali na Chunya (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa mkoa wa Mbeya Ndugu Amos Makala pamoja na kikosi kazi chakemara baada ya kupokea taarifa ya kikosi kazi cha mkoa wa Mbeya kuhusu mapendekezo ya marekebisho ya mpaka kati ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha na Vijiji kati ya Wilaya ya Mbarali na Chunya (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewaagiza Wakuu wa wilaya nchini kuchukua hatua stahiki katika kulinda na kuhifadhi mazingira katika wilaya zao ili kukabiliana uharibifu mkubwa wa mazingira kwenye misitu na vyanzo vya maji ili visikauke na kuleta athari kwa binadamu na viumbe wengine.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo mara baada ya kukabidhiwa Taarifa ya Kikosi Kazi cha Mkoa wa Mbeya na Mkuu wa mkoa wa huo Amos Makalla kuhusu Mapendekezo ya Marekebisho ya mpaka kati ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha na Vijiji katika wilaya za Mbarari na Chunya - Ikulu, Jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema tatizo la uharibifu wa mazingira katika baadhi ya wilaya nchini ni kubwa hivyo kuna umuhimu mkubwa kwa Wakuu wa wilaya kwa ushirikiano na watendaji wengine katika kukabiliana na hali hiyo kwenye maeneo yao.
Amesema kabla ya hatua kuchukuliwa ni vizuri wananchi wakaelimishwa kuhusu umuhimu wa uhifadhi wa mazingira kabla ya kuondolewa kwenye maeneo waliyovamia ikiwemo maeneo ya vyanzo vya maji.
Makamu wa Rais pia amepongeza timu ya wataalamu wa kikosi kazi cha Mkoa wa Mbeya kwa kazi kubwa na nzuri waliyoifanya inayolenga kuokoa mfumo wa ikolojia katika Bonde la Mto Ruaha Mkuu.
Kwa upande wake, Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla amemweleza Makamu wa Rais kuwa aliamua kuunda kikosi kazi hicho kwa ajili ya kushughulikia mgogoro wa mpaka kati ya wananchi wa wilaya ya Chunya na Mbarali na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, uharibifu wa mazingira na upotevu wa maji kwenye Mto Ruaha Mkuu.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla baada ya kukabidhi taarifa ya kikosi kazi kwa Makamu wa Rais amesema kikosi kazi hicho kimependekeza vijiji Tisa kati ya 33 ambavyo vina mgogoro na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha viondolewe kabisa kwenye eneo la hifadhi na vijiji vingine Vinne vinatakiwa kufutwa na wananchi kuhamishwa kwenye maeneo hayo na Serikali itawalipa fidia na kuratibu eneo watakapohamishiwa.