Kiwanda cha urafiki chaagizwa kuwalipa wafanyakazi wake mshahara
18 November 2015 | Tanzania
Mkuu wa wilaya KINONDONI, PAUL MAKONDA ameuagiza uongozi wa kiwanda cha nguo cha Urafiki cha jijini DSM, kuwalipa wafanyakazi wake mapunjo ya mshahara kutokana na uamuzi wa kesi iliyofunguliwa mwaka 2008.
Akizungumza na uongozi na wafanyakazi katika kiwanda hicho MAKONDA, amewataka wafanyakazi kusitisha mgomo na kurejea kazini huku akiuataka uongozi wa kiwanda kutekeleza amri ya mahakama ya kuwalipa wafanyakazi stahili zao. Katika hatua nyingine MAKONDA ametoa ushauri kwa serikali juu ya kuweka uwekezaji wenye tija kwa wananchi na taifa kwa ujumla.
Kiwanda cha nguo cha URAFIKI ni moja ya viwanda hapa nchini ambavyo vimekuwa vikikabiliwa na migogoro ya wafanyakazi.