Askari jela miaka 15 kwa kosa la kumuua bila kukusudia Daudi Mwangosi
27 July 2016 | Tanzania
Mahakama Kuu mjini Iringa nchini Tanzania imemhukumu jela miaka 15 askari wa kikosi cha kuzia ghasia Picifius Simon kwa kosa la kumuua bila kukusudia mwanahabari wa Daudi Mwangosi mwaka 2012.
Mwanahabari huyo alipoteza maisha wakati polisi walitumia nguvu kuwasambaratisha wafausi wa chama cha upinzani CHADEMA Wilayani Mufindi.
Jaji wa Mahakama hiyo Paul Kihwelo amesema ushahidi uliowasilishwa Mahakamani umebaini kuwa polisi huyo alitenda kosa hilo.
Jaji huyo amesema, askari alikiri kuwa alitekeleza mauaji hayi bila kudhamiria.
Hukumu hii inamaliza miaka minne ya kusubiri haki kwa familia ya Mwangosi na wanahabari nchini humo.