BAWACHA ZANZIBAR kushusha bendera
Baraza la Wanawake CHADEMA BAWACHA ZANZIBAR limepanga kushusha bendera zote za CHADEMA Kisiwani Zanzibar ndani ya masaa 24 endapo ombi lao la kurejesha viti vyao maalum katika mikoa mitano Unguja na Pemba halitazingatiwa.
Akitoa taarifa hiyo mjini Unguja mbele ya vyombo vya habari Makamu Mwenyekiti wa BAWACHA ZANZIBAR Bibi HAMIDA ABDALLAH HUWEISHI amesema wakiwa kama wanachama hai wa CHADEMA hawaoni sababu ya Baraza kuu la CHADEMA kudharau ombi hilo kutokana na Baraza hilo la CHADEMA la Wanawake limeweza kufanya kazi kubwa Zanzibar ili kuhakikisha ushindi mkubwa wa Mheshimiwa LOWASSA kupatikana.
Hivi karibuni Kaimu Katibu Mkuu wa CHADEMA SALUM MWALIMU alitangaza majina ya wabunge wawili wateule wa viti maalum kutoka katika Mikoa miwili tu ikiwa ni Unguja na Pemba jambo ambalo BAWACHA Zanzibar hawakuweza kukubaliana nalo