Home » Afrika » Mazungumzo ya kutatua matumizi ya maji ya mto Nile yaanza jijini Kinshasa

Mazungumzo ya kutatua matumizi ya maji ya mto Nile yaanza jijini Kinshasa

05 April 2021 | Afrika

Mazungumzo ya siku tatu, kutafuta mwafaka wa matumizi ya maji ya Mto Nile, yameanza jijini Kinshasa siku ya Jumamosi, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Mawaziri wa Mambo ya nje kutoka Misri, Ethiopia na Sudan wanakutana katika kikao hicho ambacho kinaongozwa na rais Felix Thisekedi ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa mataifa ya Umoja wa Afrika.

Kitovu cha mzozo wa matumizi ya maji hayo, ni hatua ya Ethiopia tangu mwaka 2011 kuanza ujenzi wa bwawa kubwa la kuzalisha umeme na inalenga kutumia maji ya mto huo.

Misri na Sudan zinasema kitendo hicho cha Ethioipia kitasababisha raia wake kukosa maji huku Misri ikisisitiza kuwa ndio chanzo chake pekee cha maji kwa watu wake madai yanayopingwa na Ethiopia.

Rais Thisekedi ambaye ameonesha nia ya kupata suluhu kati ya nchi hizo, aliwahi kutembelea Misri na Ethiopia mwezi Februari na kuahidi kupatanisha pande zote zinazokinzana.

 

Mara ya mwisho kuwepo kwa mazungumzo kama haya ilikuwa ni mwezi Januari chini ya Umoja wa Afrika, lakini hakuna mwafaka wowote uliopatikana.

/rfi

Ad