Home » Makala » Wananchi wa Kitongoji cha BINYAGO, Kijiji cha Kabegi, Kata ya Ifulifu WAMEAMUA kujenga Shule ya Msingi

Wananchi wa Kitongoji cha BINYAGO, Kijiji cha Kabegi, Kata ya Ifulifu WAMEAMUA kujenga Shule ya Msingi

21 December 2018 | Makala

Kasi ya Wananchi KUAMUA kuchangia fedha na nguvu zao kwa ajili ya ujenzi wa MIUNDOMBINU ya ELIMU na AFYA imeongezeka sana ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini.

 

Wananchi wa Kitongoji cha BINYAGO, Kijiji cha Kabegi, Kata ya Ifulifu WAMEAMUA kujenga Shule ya Msingi ambayo itaanza kutumika kama ya CHEKECHEA ifikapo April 2019. Lengo ni Shule ya Msingi Binyago ifunguliwe rasmi Januari 2020. Kwa wakati huu Darasa la Chekechea (Utayari) linasomea CHINI ya MTI.

Wananchi wanaendelea kuchanga fedha, kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji kwa ajili ya ujenzi huu.

HARAMBEE ya Ujenzi wa Shule ya Msingi Binyago imefanyika, Alhamisi, 20.12.2018 chini ya Uongozi wa Mbunge wa Jimbo Prof Sospeter Muhongo. Vifaa vya ujenzi vya kukamilisha MSINGI wa jengo (boma) la Vyumba vya Madarasa 2 na Ofisi 1 ya Walimu vimepatikana na Mbunge amechangia SARUJI MIFUKO 50. Harambee nyingine itapigwa baada ya msingi kukamilika.

MZALIWA WA KIJIJI CHA MUHOJI AAMUA KUWASHIRIKISHA WANANCHI KUJENGA ZAHANATI YA KIJIJI CHAO

Ndugu Maboto, Mzaliwa wa Kijiji cha Muhoji, Kata ya Bungwema AMEANZA UJENZI WA MSINGI wa Zahanati ya Kijijini kwao. Akimaliza ujenzi wa Msingi, Wanakijiji, Diwani Maghembe na Mbunge Prof Muhongo WAMEKUBALI KUCHANGIA ujenzi wa BOMA la Zahanati ya Kijiji hicho.

Mbunge wa Jimbo Prof Sospeter Muhongo ameendelea na ziara zake Jimboni za UKAGUZI wa Miradi ya Ujenzi na Uboreshaji wa Miundombinu ya Elimu na Afya kwenye Kata za Bugwema na Ifulifu. Ametumia fursa hiyo kuongea na wananchi na kutatua kero zao.

Wananchi wa Kata zote 2 wanaendelea kuchanga fedha, kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya ELIMU na AFYA kwenye vijiji vyao. Mbunge wa Jimbo Prof Muhongo ameendelea kukubali kuchangia miradi ya ujenzi ya wanavijiji.

Picha hapo chini zinaonyesha baadhi ya MATUKIO ya ziara za Mbunge Prof Sospeter Muhongo  ndani ya Kata za Ifulifu na Bungwema za Jimbo la Musoma Vijijini.

Ad