Home » Tanzania » MKOA WA DAR ES SALAAM KUFUNGWA KAMERA

MKOA WA DAR ES SALAAM KUFUNGWA KAMERA

15 June 2017 | Tanzania

MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM MH. PAUL MAKONDA AZINDUA MPANGO KABAMBE WA KUIMARISHA HALI YA JESHI LA POLISI MKOANI DAR ES SALAAM.

 

Na: Mwandishi wa Matokeo chanyA+

Katika awamu ya kwanza Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mh. Paulo Makonda amezindua mpango wa kukarabati Magari ya Polisi yanayotumika katika doria. Amepokea magari Mabovu 26 ambayo yamesafirishwa kwenda mkoani Kilimanjaro kuundwa upya ili kuanza kufanya kazi ya Doria. Magari hayo yatakuwa na muundo unaowawezesha askari kukaa kidoria nasio kama abiria kama ilivyosasa.

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mh. Paulo Makonda, ameahidi kukabidhi  polisi vifaa vya ulinzi kama silaha za kukamata kwa kupiga shoti ya umeme, kurunzi za mwanga mkali, bastola 500 na vikinga risasi.

Mkuu wa Mkoa wa Dae es salaam alipokuwa ziarani nchini Marekani, amepata vifaa vya patrol kwa ajili ya Jeshi la Polisi Mkoani Dar es Salaam ambavyo ni Baiskeli 500 na Pikipiki 200.

Katika awamu ya pili atakarabati na kuunda tena magari 30 na kufanya jumla yawe 56.

Amesema Katika magari hayo mara yatakapo kamilika yatafungwa Kamera za kufuatilia magari hayo na kutuma matukio yote ya barabarani Katika picha mwendo mojakwamoja makao makuu ya polisi.

Vilevile kutafungwa komputa 8 katika vituo 20 ambapo taarifa zote zinazoripotiwa zitasajiliwa kwenye computer na wahusika/watuhumiwa kuchukuliwa picha na alama mbalimbali ambazo zitahifadhiwa katika Data Centre ambayo raisi ameizindua.

Mkuu wa mkoa ameanza na vituo vya polisi 20 sasa, kutafungwa kamera ambazo zitakuwa na uwezo wa kutuma matukio mojakwa moja kwa OCD, RPC, Kamishina wa Jeshi la Polisi na kwa Mkuu wa Mkoa ambae ni Mwenyekiti wa Ulinzi na usalama wa Mkoa.

Kupitia kamera hizi wataona mubashara matukio yote yanayoendelea katika vituo vya polisi. Mtu akiiingia au akitoka polisi ataonekana.

Hatua hizi zitaondoa usumbufu kwa raia hasa wakati ndugu wanapomtafuta ndugu yao aliyekatika vituo vya polisi. Mfano ndugu aliyepotea au aliyekamatwa na kuwekwa mahabusu, hivyo hauta hangaika kumtafuta kila kituo bila mafanikio. Mwnanchi atakapo toa taarifa kituooni atataja jina na polisi watamtafuta kwa “search” tu kwenye mtandao wa jeshi la polisi kisha ataonekana kituo alipo ripoti.

Mkuu wa mkoa ametoa wito kwa wananchi kwamba siku mfumo utakapozinduliwa ni lazima taarifa ziandikwe kwenye computer na wala zisiwekwe kwenye makaratasi ambayo yalikuwa yanaleta usumbufu kwa wananchi.

Ili Kukomesha biasha za magendo, Mkuu wa mkoa amesema kwamba kutawekwa kamera hasa Katika bandari bubu, na stendi za mabasi.

Vilevile Mkuu wa mkoa amesema tayari ameanza kusimamia ufungaji wa kamera Katika jiji lote la Dar es salaam, hasa maeneo ya taa za barabarani ambazo zitasaidia sana kudhibiti makosa ya barabarani, Hivyo kutambua mienendo ya waendesha magari.

Vilevile Kamera Zitadhibiti mambo yafuatayo:-

•       Kupunguza kazi kwa askari wanaohangaika kusumbuana na waendesha magari wanaovunja sharia za barabarani.

•       Zitakomesha wizi wa kukwapuliwa pochi, mabegi, vifaa vya magari, matairi ya magari, kuvunjiwa vioo. Hivyo Vijiwe vyote vinavyouza vifaa vya magari vitasajiliwa na waeleze kwamba bidhaa wanazipata wapi?

•       Kwa kushirikiana na TTCL Kutakuwa na application (APP) maalumu ya kukuonyesha hali ya msongamano wa jiji la Dar es salaam Kiganjani mwako, Hivyo itawasaidia sana madereva kuchagua njia za kupita ili kuepusha msongamano wa magari Katika njia moja.

Pia Imeandikwa 

Ad