HAFLA YA KUKABIDHIWA RIPOTI YA VYETI FEKI
Viongozi mbalimbali wa kitaifa wameshaingia kwenye ukumbi wa Chimwaga. Yupo Katibu Mkuu Kiongozi, Waziri wa Utumishi, Mh. Angeka Kairuki, Waziri wa Elimu Prof. Ndalichako, Spika wa Bunge la JMT, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Waziri Mkuu wa JMT, Makamu wa Rais na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wameshaketi meza kuu.
Kwa ufupi Serikali yote ipo Chimwaga.
Rais Magufuli ameshawasili na wimbo wa Taifa umeimbwa.
Mama Samia Suluhu ameanza kuwasalimia wanafunzi wa UDOM.
Spika wa Bunge la JMT naye anasema maneno machache.
Anasema jinsi chuo kilivyoanza na mchango wake katika kukisimamisha chuo hiko.
Viongozi wote wanatambulishwa kwa wageni. Wako watu kutoka Baraza la Mitihani pia.
Hivi sasa mkuu wa mkoa wa Dodoma anatoa neno la ukaribisho kwa mh rais na wageni wote waliofika katika tukio hili.
Makamu Mkuu wa chuo prof. Kikula anatoa taarifa/maelezo kuhusu UDOM.
Kaimu Mkuu chuo Kikuu Dodoma
Natoa shukrani ya Dhati kwako Rais kwa kututembelea, Karibu sana.
Nasema hilo kwa dhati, shughuli za leo ungeweza kuzifanyia sehemu yoyote lakini ukazifanyia hapa.
Chuo kilianzishwa mwaka 2007. Wanafunzi wa kwanza walitahiniwa 2007 na kumaliza mwaka 2010.
Chuo kililenga kudahiri wanafunzi 40,000 na kinaendeshwa kwa mfumo wa nchini. Chuo kina shule 7.
Mafanikio.
1. Ujenzi wa miundombinu kwa viwango vya juu, shule tatu ndio bado changamoto
2. Chuo kimenzisha na kuendeleza programu 186, hakuna chuo Afrika chenye idadi hiyo
3. Chuo kimesomesha wafanyakazi wake zaidi ya 400 katika level mbalimbali kwa mapato ya ndani
4. Wahitimu wa UDOM wamefanikiwa kupata ajira sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi.
5. Chuo kimefanikiwa kuweka miundombinu ya mawasiliano kwa wizara zilizohamia Dodoma
6. Ujenzi wa Hospitali ya Benjamini Mkapa
7. Kutoa huduma kwa waathirika wa VVU
8.
Changamoto.
1. Chuo kudaiwa kodi ya Ardhi. Chuo hakina hizo hela za kulipa
2. Kutokukamilika kwa miundombinu katika shule tatu za sayansi nilizoainisha
3. Kukosekana kwa vyumba za walimu chuoni.
Matarajio.
-Chuo kina matarajio ya kudahiri wanafunzi 40,000 ikiwa changamoto hizo zitatatuliwa.
-Chuo kina matarajio ya kuendelea kukua.
-Chuo kina matarajio ya kuanzisha viatamishi (Incubators)
Si kweli kuwa kuna muingiliano kati ya Wizara zinazotumia majengo ya chuo hicho na wanafunzi wanaosoma chuoni hapo.
Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) leo kinaadhimisha miaka 10 tangu kuanzishwa kwake hafla iliyohudhuriwa na Rais Magufuli, Makamu wa Rais na PM.
Waziri wa Elimu, Prof. Ndalichako
Natoa shukrani za dhati kwa shuguli hii kufanyika Chuo kikuu Dodoma. Zipo taasisi nyingi ambazo shughuli hii ingeweza kufanyika. Wanafunzi, walimu wa Chuo wamefurahi sana ujio wako UDOM.
Ni heshima kubwa sana kwa Chuo kikuu cha UDOM.Pamoja na kuwa utapokea ripoti ya uhakiki wa vyeti pia utafungua shughuli za sherehe za miaka 10 za chuo cha UDOM
Katika wizara yangu kuna changamoto kuhusu suala la kughushi vyeti. Mwaka 2008 tulianzisha mfumo wa kuweka picha kwenye vyeti vya kitaaluma...
Kutokana na dhamira yako ya dhati Mh. Rais uliagiza watumishi wa Umma wafanyiwe uhakiki. Nashuruku mh. Kairuki aliweza kulisimamia vyema suala hili. Tunakupongeza Rais kwa kufanya maamuzi kwa vitendo.
Serikali imeziba njia zote za mkato! Wanafunzi someni, hakuna tena njia za mkato katika elimu wala ajira.
Uhakiki wa vyeti umefanyika kwa awamu tatu
1. Watumishi wa Mamlaka ya serikali za mitaa
2. Watumishi wa Taasisi na mashirika ya umma
3. Watumishi wa serikali kuu
Rais, Wizara yangu imehakiki vyeti vya kidato cha nne, sita na vyeti vya ualimu kwa watumishi wa umma.
Zoezi la uhakiki kwa awamu ya kwanza na pili umekamilika na tulikabidhi.
Uhakiki wa Vyeti vya Watumishi wa Serikali Kuu upo katika hatua za mwisho na utakabidhiwa hivi karibuni.
Napenda kuwaasa wanafunzi wa vyuo vikuu, waliojiunga vyuo vikuu either kwa kughushi au udanganyifu ni bora ukajisalimisha maana unaweza ukamaliza chuo lakini mbeleni ukakamatwa kwa vyeti feki. Majuto ni mjukuu.
Nawashukuru sana wote kwa kunisikiliza.
Waziri Ofisi ya Rais, Mh. Kairuki
Uhakiki wa aina hii haujawahi kufanyika kwa mkupuo namna hii. Mheshimiwa Rais, umeacha historia.
Tumekuwa tukibezwa sana kuwa kwanini Sensa inachukua muda mfupi lakini uhakiki unachukua muda mrefu lakini ni kwa sababu kazi hii inahitaji umakini.
Zoezi hili la uhakiki lilihusisha watumishi wa umma pekee wakiwemo Makatibu wakuu na watendaji wengine. Watumishi hawa wanatakiwa kuwa na sifa za kutumikia nafasi zao.
Zoezi hili halikuhusisha Viongozi wa Kisiasa wakiwemo Mawaziri, Wabunge, Wakuu wa Mikoa/Wilaya na Madiwani ambao wanatakiwa kujua kusoma na kuandika tu!
Ripoti hii inaonesha kuwa tayari watumishi wa Umma 400035 wamehakikiwa.
Matokeo ya uhakiki yamegawanyika kwenye makundi manne:
1. 376969 sawa na 94.23% wana vyeti halali. Baraza limehakikisha kuwa magamba ya vyeti vilivyohakikiwa vilitolewa na NECTA na taarifa zao zinaendana na zilizopo kwenye vyeti.
2. 9932 sawa na 2.4% wamebainika kuwa na vyeti vya kughushi. Vyeti vyao havifanani na vinavyotolewa na NECTA.
3. Vyeti 1538 vinatumika na zaidi ya mtumishi mmoja ambayo ni sawa na 0.3% ya vyeti vilivyohakikiwa. Hawa tunasema wana vyeti vyenye utata.
4. 11569 waliwasilisha vyeti pungufu. Hawa waliambatanisha vyeti vya utaalamu kama udaktari au ualimu pekee bila vyeti vya kidato cha nne wala cha sita.
Kwa mujibu wa kanuni ya adhabu, adhabu ya mtu aliyefanya kosa la kughushi cheti ni kifungo Jela miaka 7.
Waziri Kairuki amekabidhi ripoti na boksi lenye majina ya watumishi na taarifa zao kamili kama wako wapi na wanapatikana wapi.
Rais anatoa kitabu na kusoma jina la mtumishi mmoja " Abdallah Chanja" na kusema mengine atayasoma kwa wakati wake.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
Tunafurahi kwamba tumepata taarifa mbalimbali hapa. Siku ya Maadhimisho ya Muungano, sehemu kubwa ya waliohudhuria ni wanachuo wa UDOM.
Tunaamini kuwa elimu ni hatua na kujifunza ni mchakato. Hivyo wote wenye vyeti visivyo halali, wachukuliwe hatua. Serikali inatoa fursa mtu kuweza kurudia kidato ili kupata daraja la juu na si kupitia njia ya mkato.
Walioghushi wamepoteza sifa ya utumishi na sasa nafasi zao wapewe wahitimu wapya.
Chanzo: jf