Home » Afrika » Utafiti uliofanywa nchini DRCongo hivi karibuni

Utafiti uliofanywa nchini DRCongo hivi karibuni

26 October 2016 | Afrika

Utafiti uliofanywa nchini DRCongo hivi karibuni, unaonyesha kwamba asilimia 80,4 ya wananchi wa taifa hilo wanapinga muhula wa 3 wa rais Joseph Kabila, huku wengine wakiona kwamba kiongozi huyo anatakiwa kuondoka madarakani Novemba 19 mwaka huu.

Huku asilimia kubwa ikiona kwamba iwapo uchaguzi utafanyika nchini humo viongozi ambao hawakushiriki katika mjadala wa kitaifa uliofanyika nchini humo hivi karibuni

Kiongozi mmoja wa serikali ya DRCongo aliezungumza na RFI amesema utafiti huo hauwakilishi wananchi wote wa DRCongo na kwamba miongoni mwa watafiti hao Johson Stiens alifukuzwa nchini humo baada ya kuchapisha ripoti kuhusu mauaji ya Beni iliowaweka hatiani maafisa wa jeshi la FARDC.

Upande wake waziri wa ushirikiano na Bunge Triphon Kinkiey Mulumba amesema hajashtushwa na mitazamo ya wananchi wanaotaka mabadiliko ya kisiasa, lakini kwa hali ilivyo hakuna njia nyingine mbali na kufanyika uchaguzi huo April mwaka 2018, hivyo ni swala la viongozi kuwaelewesha wananchi.

Ad