Home » Afrika » Rais wa Rwanda Paul Kagame ametishia kuvunja upya mahusiano ya kidiplomasia kati ya Rwanda na Ufaransa

Rais wa Rwanda Paul Kagame ametishia kuvunja upya mahusiano ya kidiplomasia kati ya Rwanda na Ufaransa

12 October 2016 | Afrika

Rais wa Rwanda Paul Kagame ametishia kuvunja upya mahusiano ya kidiplomasia kati ya Rwanda na Ufaransa Mbele ya Bunge Jumatatu Oktoba 10, katika hotuba ya ufunguzi wa mwaka wa mahakama.

 

Kauli yake inatokana na hatua ya majaji wa Ufaransa kutangaza kufungua uchunguzi kuhusu mauaji ya rais wa zamani wa Rwanda Juvenal Habyarimana tarehe 6 Aprili 1994.

Mauaji hayo yanachukuliwa kama chanzo cha mlipuko wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 ambapo Washirika saba wa karibu wa Paul Kagame wanahusishwa katika mauaji hayo.

Wachunguzi wa Ufaransa wanataka kumsikia Kayumba Nyamwasa, askari wa zamani wa kijeshi wa Rwanda, aliyefarakana na Rais Paul Kagame na ambaye anamshutumu rais huyo kuwa mwanzilishi wa shambulio dhidi ya ndege ya rais Juvenal Habyarimana.

Ad