Usalama umeimarishwa kwenye mji wa Mombasa nchini Kenya
12 September 2016 | Afrika
Usalama umeimarishwa kwenye mji wa Mombasa nchini Kenya, baada ya kuuawa kwa wanawake watatu waliotekeleza shambulio la kigaidi dhidi ya Polisi wa kituo kikuu cha pwani ya Kenya.
Polisi mjini Mombasa wamesema kuwa wanawake waliohusika kwenye shambulio la kisu na bomu la kutengeneza kwa mkono, walikuwa ni raia wa Kenya na kwamba mmoja kati yao alikuwa amevalia mkanda wa mabomu ambao hata hivyo haukulipuka.