Katanga Moise Katumbi Chapwe ikiwa atarejea nchini CONGO atakamatwa
26 July 2016 | Afrika
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imesema itakamata kiongozi wa upinzani na Gavana wa zamani wa jimbo la Katanga Moise Katumbi Chapwe ikiwa atarejea nchini humo.
Katumbi ambaye ametangaza kuwania urais nchini humo yupo nje ya nchi baada ya miezi kadhaa iliyopita kwenda jijini London kutibiwa.
Serikali ya Kinshasa kupitia Waziri wake wa Sheria Alexis Thambwe Mwamba inasema itamkamata na kumfungulia mashtaka mwanasiasa huyo maarufu kwa kuhatarisha usalama wa nchi hiyo.
Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 51 ametangaza kuwa atarudi nyumbani kuendelea na harakati za kisiasa lakini hajasema atarudi lini.
|