Awamu ya pili ya mazungumzo ya amani kuhusu mzozo wa Burundi Kuanza tena
Awamu ya pili ya mazungumzo ya amani kuhusu mzozo wa Burundi, yamepangwa kurejelewa kuanza siku ya jumamosi tarehe 9 mwezi huu wa julai hadi Julai 12 mjini Arusha nchini Tanzania, lakini bila ya kushirikishwa kwa wanasiasa wa muungano wa upinzani CNARED.
Taarifa hii imechapishwa kupitia mtandao wa twitter wake Macocha Tembele, mkurugenzi wa ofisi ya mratibu wa mazungumzo hayo, rais wa zamani wa Tanzania Benjamin Mkapa.
Hatua ya kurejewa mazungumzo inakuja wakati serikali ya Burundi ikiendelea kuhamasishwa kukubali Mazungumzo kama njia ya kufikia mwafaka wa amani.
Hatua ya kutowashirikisha wapinzani wa CENARED katika mazungumzo hayo imezua hisia tofauti, siku chache baada ya kuenea taarifa kuwa mratibu wa mazungumzo hayo alikutana na wanasiasa hao mjini Brussels