Ukweli kuhusu Maxcom na TRA
Ukweli kuhusu Maxcom na TRA
LINK: https://www.youtube.com/watch?v=iJuMnecW13Y
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Maxcom Africa Ndugu Juma Rajabu amefafanua mkataba wake na Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) [CONTRACT AGREEMENT FOR THE PROVISION OF CHARGES AND TAX PAYMENT SYSTEM SERVICE AND SMS INFORMATION SERVICES. NO. AE/023/2013-14/HQ/G/001 wa Oktoba 2013.]
Akizungumza na Focus Media amesema kwamba haoni kosa lake na wala hajasikia ametajwa popote kwamba ameshindwa kutekeleza matakwa ya mkataba wake na mteja wake (TRA). Kwani anatekeleza jukumu lake na amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuondoa kero zilizokuwa zinawasibu walipa kodi nchi hasa kodi za magari. Ameongeza ukusanyaji wa mapato kwa kiasi kikubwa na inalipwa kwa wakati muafaka.
“Mambo yanayoendelea kuandikwa yenye nia ya kuichafua kampuni ya Maxcom ni chuki ya ushindani wa kibiashara kwani hata viambatanisho vilivyowekwa kwamba kuna wakubwa wanailinda kampuni sio vya kweli kwani Ukiangalia barua inayotoka kwa OS kuja kwetu iliandikwa May 19, 2014 tukiwa na miezi 6 tu kazini. Je inahusikaje kuwekwa hapa kama kielelezo kwamba “wakubwa” wanatutetea kuongezewa muda wa kufanya kazi kinyume cha sharia?” Anahoji
Mambo yanayosemwa na kuandikwa yanatakiwa yakosoe utendaji kazi wa Maxmalipo na sio kuingilia mkataba wake na mteja wake kwa kuhoji ninani amewapa kazi na wamefikaje hapo. “Wahusika (TRA) wanaweza kujibu baadhi ya maswali yanayoulizwa kwani wanafahamu utekelezaji wetu. Ninaomba jamii IPUUZE UWONGO HUU WENYE LENGO LA KUTUKATISHA TAMAA katika juhudi za kuwabana wakwepa kodi na kukusanya kodi” amasema Ndgu Rajabu.
Maxcom imesaidia sana TRA kugundua wamiliki wa Kadi bandia za kumiliki magari ambao walikuwa wakizitumia katika malipo bandia kwa kukwepa kodi.
Vilevile Maxcom ndio waliobuni mfumo wa kutoza faini za papokwahapo kwa kutumia mashine maalum barabarani. Mifumo ambayo imelisaidia sana jeshi la polisi kuongeza mapato yake ambayo wanayaona. Vilevile mfumo huu unawaondoa watumiaji wa leseni bandia za Udereva waliokuwa wanaikosesha serekali mapato.
Mafanikio mengine ni kuwezesha ukusanyaji wa mapato na ulipaji wa kodi kupiti a mabasi yaendeyo kasi (UDART), vivuko mbalimbali nchini kama Magogoni na Busisi Mkoani Mwanza mabako mapato yameongezeka kwa kiasi kikubwa, na tumerahisisha manunuzi ya umeme (LUKU) maji na huduma nyingine nyingi kwakutumia simu ya mkononi au Mawakala wa Maxmalipo nchi nzima.
Hata hivyo amepongeza jitihada za Rais wa jamhuri ya muungano ya Tanzania Dr. Magufuli za kukusanya kodi na jinsi anavyoamini kwamba nchi hii haitakiwi kuwa tegemezi bali inatakiwa kuwa nchi ya kutoa misaada.
Amefafanua kwamba Maxcom Africa ltd inauwezo wa kuhakikisha kwamba mapato yanakusaywa moja kwa moja kwenda TRA bila TRA kuendelea kusubiri wakusanyaji wapeleke mapato TRA, kwani mara nyingine yanacheleweshwa kufika serekalini kwa sababu za kibinadamu. Amesema inawezekana kwamba mapato yanayotakiwa kulipwa serekalini yanalipwa mojakwamoja kutoka kwa Mnunuzi yanafika TRA kwa wakati kwa njia ya mtandao popote nchini.
Hivyo amemuomba Mheshimiwa Rais azidi kuwapa Fursa zaidi wazawa washirikiane na Serekali ili kukusanya mapato ya ndani kwa lengo la kufika kule tunapotarajia.
Kampuni ya maxcom Africa Ltd kwa sasa imetoa ajira rasmi zaidi ya mia tano (500) na ajira zisizo rasmi zaidi ya elfu ishirini (20,000) kote nchini, zikiwa ni ajira kwa wakala, wafanyakazi katika vituo mbalimbali vya usafiri na usafirishaji kama ferry, DART na sehemu mbalimbali za malipo.
Hivi sasa maxcom Afica ltd inafanya kazi katika nchi nyingine kama Uganda, na Rwanda (MaxPay)