Home » Tanzania » NIDA ya kwanza katika Maadhimisho ya Maonyesho ya 40 ya Kibiashara Kimataifa

NIDA ya kwanza katika Maadhimisho ya Maonyesho ya 40 ya Kibiashara Kimataifa

01 July 2016 | Tanzania

Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa imeibuka Mshindi wa kwanza katika Maadhimisho ya Maonyesho ya 40 ya Kibiashara Kimataifa – Sabasaba kama Banda Bora katika Kutoa Huduma Bora na yenye Viwango kwa Umma inayotoa mchango katika Kuwezesha Kuunganisha Biashara na Masoko pamoja na Uwekezaji (Best Exhibitor Trade and Investment Support Dar Es Salaam International Trade Fair – DITF) yaliyoanza tarehe 28/06/2016 – 08/06/2016

Kupitia Utambulisho; NIDA inakusudia kuunganisha biashara na masoko kupitia Kanzi data (database) ambayo itaunganisha mifumo yote ya Serikali na Binafsi katika utoaji huduma. Zipo huduma ambazo tayari zimeanza kutumia mfumo wa Nida katika utoaji huduma ikiwemo sekta ya Benki

Zipo faida nyingi za kuwa na Kitambulisho cha Taifa kiuchumikisiasa ,kijamii na Kiulinzi na Kiusalama.

Katika maonyesho ya 40 ya Kimataifa Sabasaba mwaka huu, huduma ambazo zinatolewa ni Usajili wa moja kwa moja kwa wananchi ambao hawana vitambulisho, kusoma taarifa za mwananchi zilizopo kwenye kadi, kutoa ufafanuzi kuhusu matumizi ya vitambulisho yanayokusudiwa pamoja na kuonyesha njia mbalimbali zinazotumika kusoma taarifa zilizomo kwenye kadi.

Ad