Home » Tanzania » Baada ya kulipa kodi, Kiwanda cha DANGOTE kimeruhusiwa kuingiza Makaa ya mawe na Gypsum

Baada ya kulipa kodi, Kiwanda cha DANGOTE kimeruhusiwa kuingiza Makaa ya mawe na Gypsum

21 June 2016 | Tanzania

Wizara ya Nishati na Madini imeipatia kampuni ya Saruji ya Dangote mkoani Mtwara vibali kuruhusu meli mbili zinazoingiza makaa ya mawe na gypsum kupakua ili zitumike kiwandani hapo baada ya kukamilisha utaratibu wa kuzilipia kodi ya ongezeko la thamani (VAT) ya zaidi ya shilingi Bilioni mbili.

Pesa hizi na pamoja na malimbikizo ya malipo ya Ongezeko la thamani (VAT) ya makaa ya mawe  yaliyoingia mwezi wa kumi na moja mwaka jana (2015)

Meli hizo zilizo zuiliwa kwa zaidi ya siku 18, zilikuwa zikiingiza nchini Mkaa ya mawe na gypsum kwa ajili ya kuendeshea mitambo ya kutengeneza saruji na kutengeneza saruji katika kiwanda cha Dangote Cement Mjini Mtwara.

Vibali  hivyo kamishina wa madini vinaruhusu kampuni ya dangote kuingizwa kwa Mita za ujazo 34,881Mt za Gypsum na Mita za ujazo 38,000Mt za makaa ya mawe.

Kampuni ya Dangote imeandika barua ya makubaliano iliyoandikwa tarehe 20 juni 2016 ya kununua makaa ya mawe na gypsum inayopatikana hapa Tanzania,

Hata hivyo kampuni ya Dangote imelipa ushuru wa forodha wa zaidi ya shilingi milioni 50, katika bandari ya Mtwara, ili kuingiza makaa ya mawe na Gypsum.

Kamishna mkuu wa TRA Alphayo Kidata, akizungumza na mwandishi wa habari hizi amesema kwamba ni kweli Kiwanda cha Dangote wamelipa VAT ya bidhaa wanazoingiza na wamesha ruhusiwa na kamishna wa madini kupakua meli hizo.

Vile vile amawashauri wazalendo kufichua wale wote wanaokwepa kulipia kodi bidhaa wanazoingiza nchini, kwani kwa kutoa taarifa ambazo zitafanikisha TRA kupata kodi yake, kuna asilimia ambayo hutolewa kama zawadi kwa walitoa taarifa na TRA wakafanikisha kupata kodi hiyo.

 

Ad