Kizza Besigye anayezuiliwa kwa kosa la uhaini ashtakiwe Mahakamani
15 June 2016 | Afrika
Mahakama jijini Kampala nchini Uganda, imeamua kuwa kingozi wa upinzani kutoka chama cha FDC Kizza Besigye anayezuiliwa kwa kosa la uhaini ashtakiwe Mahakamani, sio katika Gereza la Luzira kama serikali inavyotaka.
Kiongozi wa mashtaka amekuwa akishindwa kumfikisha Mahakamani Dokta Besigye kuanzia mapema mwezi huu kwa madai kuwa kufanya hivyo kutahatarisha hali ya usalama.
Besigye aliwasilishwa Mahakamani leo asubuhi katika Mahakama ya Nakawa chini ya ulinzi mkali, huku Hakimu wa Mahakama hiyo James Ereemye akimtaka kiongozi wa mashtaka kukamilisha uchunguzi dhidi ya Besigye kufikia tarehe 29 mwezi huu keis hiyo itakaporejelewa.