Home » Tanzania » Rais Magufuli ameagana na Balozi wa Italia hapa nchini Mheshimiwa Luigi Scotto

Rais Magufuli ameagana na Balozi wa Italia hapa nchini Mheshimiwa Luigi Scotto

07 June 2016 | Tanzania

Rais Magufuli ameagana na Balozi wa Italia hapa nchini Mheshimiwa Luigi Scotto ambaye amemaliza muda wake wa miaka mitatu.

Balozi Luigi Scotto amesema katika kipindi chake amewezesha kuongezeka kwa biashara kati ya Italy na Tanzania kwa asilimia 35 na ameielezea Tanzania kuwa ni nchi nzuri aliyoipenda na kwamba ataendelea kutangaza fursa zilizopo Tanzania huko Italia na kwingineko.

Mapema leo asubuhi, Rais Dkt. John Pombe Magufuli ametia saini kitabu cha maombelezo katika Ofisi ya Ubalozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Nchi za Kiarabu ya Saharawi iliyopo Mikocheni Jijini Dar es salaam, kufuatia kifo cha Rais wa nchi hiyo Mohamed Abdelaziz aliyefariki dunia Jumanne iliyopita tarehe 31 Mei, 2016.

Rais Magufuli ambaye amepokelewa na Balozi wa Saharawi hapa nchini Mhe. Brahim Salem Buseif amesema Marehemu Mohamed Abdelaziz ambaye pia alikuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Polisalio Front, atakumbwa kwa juhudi zake za kupigania ukombozi na uhuru wa Saharawi.

"Kwa niaba ya Serikali na wananchi wa Tanzania napenda kutoa salamu zangu za pole kwa Serikali na wananchi wa Saharawi kwa kumpoteza kiongozi ambaye alijitoa kwa ajili ya kupigania ukombozi na uhuru wa Jamhuri ya Saharawi.

"Namuombea kwa Mwenyezi Mungu, aipumzishe roho yake mahali pema peponi, Amina" Amesema Dkt. Magufuli katika salamu hizo.

 

Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Dar es salaam

06 Juni, 2016

Ad