Mwanafunzi mmoja wa kike alipata mushtuko wa moyo
20 April 2016 | Afrika
Mwanafunzi mmoja wa kike alipata mushtuko wa moyo alipokamatwa pamoja na wenzake wawili na maafisa wa polisi katika Chuo Kikuu cha Rhodes nchini Afrika Kusini wakati wakiandamana kulaani visa vya ubakaji vinavyoendelea katika Chuo chao.
Ripoti zinasema kuwa, mwanafunzi aliyepata mshtuko huyo alikibizwa hospitalini kupata matibabu.
Wanafunzi hao wa kike walikuwa wanaandamana wakitaka wanafunzi 11 wa kiume kuchukuliwa hatua ya Chuo hicho kwa madai ya kuhusika na ubakaji na visa vingine vya unyanyasaji wa kimapenzi dhidi ya wanafunzi wa kike.
Mkuu wa Chuo hicho Sizwe Mabizela alijitahidi kuwaomba polisi kuacha kutumia nguvu na kuwaachilia wanafunzi hao bila mafanikio.