Waziri mkuu Kasim Majaliwa amemsimamisha kazi daktar Mtwara
Waziri mkuu Kasimu Majaliwa amemsimamisha kazi daktari mmoja wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mtwara, Ligula baada ya kufuatia tuhuma za kumuomba mgonjwa rushwa ya shilingi laki moja na kumuandikia dawa ambazo hazijatumika.
Aidha ameagiza maduka ya dawa yaliyopo karibu na hospitali hiyo kufungwa mara moja baada yeye kuondoka katika eneo la hospitali kutokana na madaktari kujihusisha na biashara na kuacha kutumia dawa za serikali zilizopo katika hospitali hiyo.
Akiwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya mashujaa mkoani Mtwara,waziri mkuu Kasimu Majaliwa baada ya kuzungumzia changamoto za afya wananchi kwa kupaza sauti wakamuomba kutembelea hospitali ya rufaa ya ligula ya mkoa wa mtwara ili akatumbue majipu.
Baada ya maombi hayo leo hii akatembelea hospitali hiyo ambapo napo alikutana na wananchi wakiwa wanaimba na kueleza kero zao.
Kutokana na kupata malalamiko hayo kutoka kwa wananchi na kukagua wodi mbalimbali katika hospitali hiyo Waziri mkuu Kasimu Majaliwa anamsimamisha kazi dokta Fortunatusi Namahala na kuagiza uchunguzi ufanyike juu yake.
Aidha kuwepo kwa malalamiko ya wagonjwa kuelekezwa na madaktari kwenda kununua dawa katika maduka yaliyopo nje ya hospitali hiyo waziri mkuu anatoa agizo.