Kizza Besigye amesema hana imani na uchaguzi
Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Uganda, FDC, amesema hana imani na uchaguzi utakaofanyika juma hili ikiwa utakuwa huru na haki na kulituhumu jeshi la polisi nchini humo kwa kuchochea vurugu kuelekea uchaguzi mkuu.
Kizza Besigye, kiongozi wa upinzani kwa muda mrefu aliyeshindwa kwenye chaguzi tatu zilizopita, amewaambia waandishi wa habari kuwa licha ya kuwepo matumaini makubwa kwa wananchi kuona mabadiliko baada ya miongo mitatu ya utawala wa rais Yoweri Museveni, matumani hayo hayapo tena kwasasa kutokana na vitendo inavyofanyiwa kambi ya upinzani.
Besigye ameongeza kuwa ndio maana hata jana polisi wa Uganda walitumia nguvu kuwatawanya wafuasi wake na kuharibu ratiba ya kampeni zake alizokuwa amepanga kuzianya katikati ya jiji la Kampala, na kwamba hakuna fursa yoyote ya uchaguzi wa juma hili kuwa huru na wa haki.