Kurejeshwa nchini Burundi, maofisa watatu wa jeshi
Nyaraka za siri zilzizopatikana, zimeonesha kuwa mkuu wa tume ya walinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, ameagiza kurejeshwa nchini Burundi, maofisa watatu wa jeshi la nchi hiyo kwa tuhuma za kuhusika na vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu.
Katika barua ya siri iliyoandikwa February 5 kwa kitengo cha operesheni za walinda amani cha umoja wa mataifa na kuelekezwa kwa mkuu wa tume ya walinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya kati MINUSCA, ilieleza ni kwanini wanajeshi hao wa Burundi wanarudishwa nyumbani.
Maofisa hao wamerudishwa nyumbani baada ya kubainika kuwa walihusika katika kutekeleza vitendo vya unyanyasaji na mateso dhidi ya waandamanaji nchini Burundi waliokuwa wakipinga muhula watatu wa rais Pierre Nkurunziza.