Home » Afrika » Mkuu wa zamani wa jeshi la Kongo kuwania nafasi ya urais katika uchaguzi wa Machi 20

Mkuu wa zamani wa jeshi la Kongo kuwania nafasi ya urais katika uchaguzi wa Machi 20

09 February 2016 | Afrika

Mkuu wa zamani wa jeshi la Kongo na mshauri wa rais ametangaza  mpango wa kuwania nafasi ya urais katika uchaguzi wa Machi 20 kukabiliana na Rais wa sasa Denis Sassou Nguesso, ambaye amekuwa madarakani nchini Congo-Brazzaville kwa zaidi ya miaka 30.

Jenerali  Jean-Marie Michel Mokoko ameiambia AFPkwa njia ya simu akiwa mjini Bangui kuwa anajisikia kuitwa kuwatumikia wananchi na ameamua kuingia ulingoni kugombea.

Mokoko ambaye ni kwa sasa ni mwakilishi maalum wa Tume ya Umoja wa Afrika nchini Jamhuri ya jirani ya Afrika ya Kati anasema anaifahamu nchi yake vizuri , changamoto zake na  historia yake hivyo anaamini anaweza kuongoza

 

Ad