Huko nchini Kenya mcheza kamari raia wa Tanzania ameuawa
Huko nchini Kenya mcheza kamari raia wa Tanzania ameuawa na kundi la watu kwa kupigwa mawe,baada ya kuwaua watu wawili kufuatia kupoteza pesa zake katika mchezo huo na kushindwa kukubaliana na hali hiyo, polisi wamesema leo Jumanne.
Mtanzania huyo alipandwa na hasira baada ya kupoteza dola 300 katika casino moja wilayani Eastleigh mjini Nairobi majira ya asubuhi leo Jumanne, na kumshambulia meneja wa casino baada ya kukataa kumkopesha fedha ili aendelee kucheza.
Kwa mujibu wa mkuu wa polisi jijini Nairobi Japhet Koome,mtu huyo baada ya kunyimwa pesa aliondoka na kurejea na panga na kumshambulia meneja huyo mwanamke na kumwua kisha akamvamia mlinzi ambaye alijaribu kuingilia na kumua pia kabla ya kukamatwa na wacheza kamari wenzie na kumwua kwa kupiga mawe