Home » Afrika » Mawakili wa mashtaka Burundi wamekata rufaa kesi ya jaribio la mapinduzi

Mawakili wa mashtaka Burundi wamekata rufaa kesi ya jaribio la mapinduzi

04 February 2016 | Afrika

Version:1.0 StartHTML:0000000167 EndHTML:0000002672 StartFragment:0000000457 EndFragment:0000002656

Mawakili wa upande wa mashtaka nchini Burundi wamekata rufaa dhidi ya hukumu ya viongozi wa jaribio la mapinduzi wakitaka viongozi hao kupatiwa adhabu ya kifungo cha maisha jela ikiwa ni pamoja na wale saba walioachiwa huru.

 

Mawakili hao Pia walitoa orodha ya majina 34 ya viongozi wa upinzani na wa vyama vya kiraia na waandishi wa habari ambao kwa sasa wapo uhamishoni wakitaka wakabiliwe na mkono wa sheria kwa kuhusika katika jaribio la mapinduzi ya Mei 2015.

 

Rufaa hiyo inakuja baada ya mahakama mnamo mwezi january kuwafunga wanaume 21 waliohusika katika jaribio la mapinduzi huku magenerali wanne wa zamani wakihukumiwa kifungo cha maisha tisa wengine miaka 30 jela na wanajeshi 8 kifungo cha miaka 5 jela.

 

Mawakili wa upande wa mashtaka wamedai kutoridhishwa na hukumu iliyotolewa awali na kutaka wahusika wote kupatiwa adhabu ya kifungo cha maisha jela huku wale saba walioachiwa huru kesi yao kurejelewa.

 

Burundi imekuwa katika mgogoro wa kisiasa tangu April 2015 baada ya raisi Pierre Nkurunziza kuwania nafasi hiyo kwa mara nyingine na kusababisha maandamano ya kumpinga na jaribio la mapinduzi yaliyoshindwa mauaji mfululizo na uasi.

Ad