Waziri mkuu Matteo Renzi ameionya nchi ya Misri
12 February 2016 | Nje ya Afrika
Wakati Serikali ya Italia ikimzika raia wake Giulio Regeni, waziri mkuu Matteo Renzi ameionya nchi ya Misri na kusema kuwa urafiki wao uko mashakani kutokana na uchunguzi wao kushindwa kueleza ni namna gani raia wake aliuawa.
Waziri mkuu Renzi amesema Serikali ya Misri ilitoa ushirikiano kwenye madai yake kwamba wachunguzi wa nchi yake wahusishwe kufanya uchunguzu kuhusu kifo cha Regen ambaye mwili wake ulipatikana ukiwa na majeraha yanayoenesha ishara kuwa aliteswa kabla ya kuuawa.
Waziri mkuu wametoa pole kwa familia ya Regen, na kuongeza kuwa ameiandikia barua Serikali ya Misri na kuileza kuwa urafiki ni kifaa muhimu lakini urafiki huo unaweza kuendelea ikiwa kuna ukweli.