Home » Nje Ya Afrika » Raia Marekani walioachiwa huru na Iran wamewasili nchini Ujerumani

Raia Marekani walioachiwa huru na Iran wamewasili nchini Ujerumani

18 January 2016 | Nje ya Afrika

Raia watatu wa Marekani walioachiwa huru na utawala wa Iran kama sehemu ya mabadilishano ya wafungwa, wamewasili nchini Ujerumani ambapo wanatarajiwa kusafirishwa hadi kwenye kambi ya kijeshi ya Marekani.

Wafungwa hawa wote walioachiwa wana uraia wa nchi mbili za Iran na Marekani, waliwasili nchini Ujerumani saa chache baada ya kutua kwa muda mfupi mjini Geneva Uswis, ambapo watakuwa Ujerumani kwaajili ya uangalizi wa kiafya kabla ya kurejea nyumbani.

Kati ya wafungwa hao yupo mwandishi wa habari wa gazeti la Jason Rezaian ambaye alikuwa akishikiliwa nchini Iran kwa zaidi ya miezi 18, wamo pia, Christian Pastor Abedini na mwanajeshi wa zamani wa Marekani, Amir Hekmati.

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani John Terry amethibitisha kuachiwa kwa wafungwa hao na kuongeza kuwa wapo wafungwa wengine wawili ambao wameachiwa na utawala wa Iran katika mpango mwingine wa makubaliano kati ya nchi hizo mbili.

Katika hatua nyingine saa chache baada ya Iran kuondolewa vikwazo na nchi za Magharibi kutokana na kutimiza masharti ya kupunguza urutubishaji wa Urani, Marekani imetangaza vikwazo vipya baada a nchi hiyo kutekeleza jaribio la kombora la masafa marefu.

Ad