Polisi nchini Indonesia imekamata meli 27
Polisi nchini Indonesia imekamata meli 27 za kigeni zilizokuwa zikifanya uvuvi haramu, katika hatuwa ya kupambana na Uvuvi haramu. Miongoni mwa meli zilizokamatwa ni pamoja na meli kutoka Ufilipino, Vietnam, Malaisia na Myanamar.
waziri anaehusika na maswala ya Uvuvi nchini Indonesia Susi Pudjiastuti amesema meli hizio zilikamatwa zote zikifanya uvuvi kinyume cha sheria katika eneo la indonesia, huku meli nyingine nne za Indonesia zikikamatwa kwa kufanya shughuli za uvuvi bila kibali.
Waziri huyo ameendelea kusema kuwa, serikali imechukuwa hatuwa madhubiti katika kuheshimisha sheria za ulinzi wa maji na usalama.
Katika hatuwa nyingine, kundi la waislam wenye msimamo Mkali waliokamatwa hivi majuzi wakati wakiwa katika mafunzo ya kijeshi kwenye kisiwa kimoja kilicho sahaulika nchini humo, wameanza kuhojiwa kabla ya kufikishwa mahakamani.
watu zaidi ya 30 wanaominika kuwa ni waislam wenye msimamo mkali walitiwa nguvuni katika operesheni ya polisi kwenye kisiwa cha Sunbing, huku wengine watano waliokuwa wakifuatiliwa tangu kipindi kadhaa wakikamatwa katika eneo la Malang, duru za polisi zimethibitisha
hakuna uhusiano wowote uliobainishwa kati ya kukamatwa huko na mashambulizi ya Kigaidi ya mjini Jakarta yaliotekelezwa na wapiganaji wa kundi la Islamic State mwezi Januari iliopita.
Kiongozi mmoja wa polisi katika operesheni hiyo ambae hakupenda jina lake litajwe amesema wameshambulia maeneo ya milima wakati wa operesheni zao wa silaha baada ya kupewa taarifa na raia wema waliokuwa wakisikia milio ya risase katika kisiwa hicho.
Duru zaidi zinaeleza kuwa watu hao ni kutoka katika kundi la waislam wenye msimamo mkali la Jamaah Ansharus Syariah.