Home » Nje Ya Afrika » Obama na mwenzake Rouhani, wamepongeza hatua ya kihistoria iliyofikiwa

Obama na mwenzake Rouhani, wamepongeza hatua ya kihistoria iliyofikiwa

18 January 2016 | Nje ya Afrika

Rais wa Marekani Barack Obama na mwenzake wa Iran Hassan Rouhani, wamepongeza hatua ya kihistoria iliyofikiwa mwishoni mwa juma ambapo nchi za Magharibi zimetangaza kuiondolea vikwazo vya kiuchumi nchini ya Iran baada ya tangazo la tume ya umoja wa mataifa ya Atomic IAEA kuthibitisha Iran kutimiza masharti ya kupunguza urutubishaji wa

IAEA ilitangaza siku ya Jumamosi kuwa baada ya waangalizi wake kufanya ziara nchini Iran na kutembelea vinu vyake vya nyuklia, waliridhika kuwa nchi hiyo kwa sehemu kubwa imetekeleza matakwa ya nchi za Magharibi kuhusu matumizi ya Urani.

Hata hivyo licha ya rais Obama kusifu mpango huo, akaonya kuwa nchi yake haitasita kuichukulia hatua kali Iran iwapo itabaini kuwa taifa hilo limekiuka makubalino yao kuhusu mpano wake wa nyuklia.

Waziri mkuu wa Israel, Benjamini Netanyahu hapo jana ameendelea kusisitiza kuwa nchi yake inataarifa za kina kuhusu Iran kuendelea na mpango wake wa nyuklia, na kutaka hatua kali zaidi kuchukuliwa dhidi ya Iran iwapo itabainika kukiuka sharti lolote kwenye mkataba uliofikiwa.

Nchi ya Iran sasa itakuwa na uwezo wa kuchukua fedha kwenye mabenki ya nje ambayo yalizuia fedha zake ikiwa ni pamoja na kuruhusiwa kuuza mafuta katika soko la dunia, hatua ambayo wananchi wengi wa Iran imewapa ahueni ya kiuchumi.

Ad