Mgombea urais wa Marekani Donald Trump hatashiriki mjadala
27 January 2016 | Nje ya Afrika
Mgombea urais wa Marekani anayewania kuchaguliwa na chama chake cha Republican Donald Trump hatashiriki mjadala wa siku ya Alhamisi unaorusha kwa njia ya televisheni, hatua inayokuja siku nne tu kabla ya jimbo la Iowa kuanza mchakato wa uteuzi.
Trump anayewania kuteuliwa na chama chake, aliweka hadharani wazo lake la kujiondoa katika mjadala huo wakati wa kampeni jana Jumanne huko Iowa, ambapo alisema, kuwa bila shaka hatashiriki mjadala.
Kauli hiyo ilithibitishwa punde baada ya kampeni zake katika kauli nzito kwamba Bwana Trump hujua mpango mbaya anapobaini mmoja, kauli iliyoelekzwa kwa Shirika la habari la Fos na mwendesha mjadala wa Iowa ambaye Trump anamshutumu kwa upendeleo