Kansela kuguswa na hali ya kibinadamu inayoshuhudiwa nchini Syria
17 February 2016 | Nje ya Afrika
Kansela wa ujerumani Angela Merkel ameeleza kuguswa na hali ya kibinadamu inayoshuhudiwa nchini Syria na kudai kuwa haivumiliki na kurelejea wito wake wa kupiga marufuku ndege za kivita kuruka maeneo ya raia.
Kiongozi huyo ameongeza kuwa mashambulizi ya anga yanayoungwa mkono na Urusi mjini Alepo yamesababisha wakazi wengi kukimbia kaskazini mwa syria.
Merkel ameliambia bunge la ujerumani kuwa ingekuwa afadhali kama kungekuwa na maeneo maalum ambayo makundi yanayoshiriki katika vita yangekuwa hayafiki na kushambulia.
Kwa mujibu wa Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kuhusu Syria Staffan de Mistura amesema misaada ya chakula inapelekwa kwa majaribio katika miji iliyoathirika.