Home » Nje Ya Afrika » Hillary Clinton kuwa mgombea urais katika historia ya nchi ya Marekani

Hillary Clinton kuwa mgombea urais katika historia ya nchi ya Marekani

27 July 2016 | Nje ya Afrika

Hillary Clinton ameweka historia kwa kuwa mwanamke wa kwanza kuidhinishwa kuwa mgombea urais katika historia ya nchi ya Marekani.

Ni rasmi sasa kuwa Seneta huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 68, atapambana na mgombea wa Republican Donald Trump wakati wa uchaguzi mkuu mwezi Novemba mwaka huu.

Clinton alihitaji wajumbe 2,382 kuidhinishwa kwa mgombea wa Democratic, idadi ambayo iliipata baada ya kupitishwa na wajumbe wote.

Baada ya uteuzi huo rais wa zamani na mume wa mgombea huyo Bill Clinton, aliwahotubia maelfu ya wajumbe hao katika mkutano huo unaoendelea kwa siku ya tatu leo katika mji wa Philadelphia.

Leo itakuwa zamu ya Rais Barrack Obama na Makamu wake Joe Biden, na mgombea mwenza wa Bi.Clinton Tim Kaine, kuwahotunia wajumbe hao.

Hillary Clinton naye anatarajiwa kuwa mzungumzaji wa mwisho hapo kesho atakapokubali uteuzi huo.

 

Ad