Home » Biashara » FOCUS MEDIA Tunapinga Matumizi ya dawa za Kulevya

FOCUS MEDIA Tunapinga Matumizi ya dawa za Kulevya

14 February 2017 | Biashara

Utegemezi wa dawa za kulevya ni hali ya kuugua au isiyo ya kawaida ambayo hutokana na matumizi ya dawa ya mara kwa mara.

Tatizo la dawa za kulevya linahusisha uendelezaji matumizi sugu ya dawa hadi kufikia tabia ya kutafuta dawa za kulevya, kuwa katika hatari ya kurejelea matumizi na upungufu wa uwezo wa kukabiliana na visisimuaji vya kuridhisha kwa kawaida.

Mwongozo wa Utambuzi na Takwimu ya Matatizo ya Akili (DSM-IV) imebainisha hatua tatu za utegemezi wa dawa za kulevya: kujihusisha/kutarajia, unywaji/ulevi, na kuacha/athari mbaya .

Sifa za hatua hizi hudhihirika mtawalia, kila mahali, kwa utashi wa mara kwa mara na ujihusishaji na kutafuta vileo; matumizi zaidi ya vileo kuliko inavyohitajika kufikia madhara ya kulevya , na kufikia uzoelevu, dalili za kujiondoa na upungufu wa motisha kwa shughuli za kawaida za kimaisha.

Kulingana na ufafanuzi wa Shirika la Marekani la Tiba za Ulevi, utegemezi wa dawa za kulevya hutofautianana utegemeaji wa dawana uzoevu wa dawa za kulevya.

Ni jambo la kawaida kabisa kati ya wanasayansi na waandishi wengine , kuruhusu dhana ya matumizi ya dawa za kulevya kujumuisha watu ambao si watumiaji dawa za kulevya, kulingana na ufafanuzi wa Shirika la Marekani la Tiba za Ulevi . Neno utegemezi wa dawa za kulevya hatimaye hutumika kama kategoria ambayo inaweza kujumuisha wale watu ambao, chini ya DSM-IV, wanaweza kutambuliwa kama wategemezi wa vileo au watumizi wa vileo hivi vibaya . (Tazama pia DSM-IV codes)

Istilahi matumizi mabaya na uzoelevu wa dawa za kulevya zimeweza kufafanuliwa na kufafanuliwa upya kwa miaka mingi. Kamati ya Wataalamu wa Shirika la Afya Duniani ya 1957 (WHO) kuhusu dawa zinazosababisha utegemeaji wa kulevya walifafanua-utegemezi kwa vileo na uzoevu kama sehemu ya matumizi mabaya ya dawa za kulevya:

Matumizi ya dawa za kulevya ni hali ya ulevi wa muda au wa kila mara unaotokana na matumizi ya mara kwa mara ya dawa (asili au sanisi). Sifa zake ni pamoja na: (i) utashi mkubwa au uhitaji (wa kimazoea) wa kuendelea kutumia dawa ya kulevya na kuitafuta kwa njia yoyote ile; (ii) tabia ya kuongeza kiwango, (iii) utegemeaji wa kiakili (kisaikolojia) na wa kimwili kwa jumla kwa athari za dawa za kulevya, na (iv) athiri mbaya kwa mtu binafsi na kwa jamii.

Uzoevu wa dawa (tabia) ni hali inayosababishwa na matumizi ya mara kwa mara ya dawa za kulevya. Sifa zake ni pamoja na (i) utashi (lakini siyo ya kimazoea) wa kuendelea kutumia dawa za kulevya kwa minajili ya kuhisi ustawi wa kihali ambayo huibushwa; (ii) tabia ya kuongeza kiwango kidogo au kutoongeza , (iii) kiasi fulani cha utegemeaji wa kiakili kwa athari za dawa za kulevya, lakini bila ya utegemezi wa kimwili na hivyo ni wa dalili za kuacha [kujiondoa], na (iv) madhara mabaya, iwapo yapo, hasa kwa mtu binafsi.

Katika mwaka wa 1964, kamati mpya ya WHO iligundua kuwa fafanuzi hizi ni duni, na kupendekeza matumizi ya istilahi ya kijumla ya "utegemezi wa dawa za kulevya":

Ufafanuzi wa neno kulevya ulipata ukubalifu, lakini utata katika matumizi ya istilahi matumizi ya dawa za kulevya na uzoevu na matumizi mabaya uliendelea. Aidha, orodha ya dawa za zilizotumika vibaya iliongezeka kiidadi na kwa wingi. Utata huu umezidi kubainika wazi na jitihada mbalimbali zimefanywa kutafuta istilahi inayoweza kutumika kwa ujumla kuelezea matumizi mabaya ya dawa za kulevya . Dhana ya kimsingi katika yote mawili inaonekana kuwa utegemezi, ama wa kiakili au wa kimwili . Kwa hivyo, matumizi ya neno 'utegemezi wa dawa , yanayojumuisha awamu ya kimpito huihusisha na aina mahususi ya dawa ili kutofautisha aina moja ya dawa ya kulevya na nyingine, yalipewa uzingativu wa makini sana. Kamati ya wataalamu inapendekeza matumizi ya neno 'utegemeaji wa dawa' badala ya 'matumizi ya dawa za kulevya' na 'uzoevu wa dawa za kulevya'.

Kamati hiyo haikufafanua kikamilifu utegemezi, bali aliendelea mbele na kubainisha kuwa palikuwa na tofauti kati ya utegemezi wa kimwili na kisaikolojia ("kiakili"). Ilieleza kuwa matumizi mabaya ya dawa za kulevya ilikuwa"hali ya utegemezi wa kiakili au utegemezi wa kimwili, au yote mawili, kwa dawa za kulevya, ambayo hudhihirika kwa mtu kufuatana na matumizi ya dawa hiyo kwa vipindi vifupi au vinavyodumu kwa muda." Utegemezi wa kiakili ulifafanuliwa kama hali ambapo "pana hisia za kuridhika na msisimko wa kiakili ambao huhitaji matumizi ya dawa ili kuibusha raha au kuepusha usumbufu" kwa muda mfupi au muda mrefu " na dawa zote za kulevya zilisemekana kuwa na uwezo wa kuibusha hali hii:

Ni nadra sana kupata hali ambapo kitu chochote kinachoingizwa mwilini kitashindwa kuwasababisha baadhi ya watu kuathirika kwa msisimko wa kuridhika au kufurahia, kwa namna inayowashawishi kuendeleza matumizi yake hadi kufikia kiwango cha matumizi mabaya - yaani, kutumia kupita kiasi au kutumia zaidi ya invyohitajika kimatibabu.

Fafanuzi za miaka ya 1957 na 1964 za matumizi ya dawa za kulevya, utegemezi na utumiaji mbaya zimeendelea kudumu hadi sasa katika vitabu vya kimatibabu. Inafaa kukumbukwa kuwa wakati huu (2006) Mwongozo Utambuzi wa Takwimu (DSM-IV-TR)kwa sasa unatoa vigezo maalum vya kufafanulia matumizi mabaya na utegemezi. (DSM-IV-TR) hutumia istilahi utegemezi wa vileo badala ya matumizi ya vileo, ambao ni uigaji mbaya wa mkondo wa matumizi mabaya ya vileo, unaosababisha kuathirika vibaya kiafya au dhiki, kama ionekanavyo kwa vigezo vitatu (au zaidi) vilivyopendekezwa , kuanzia wakati wowote katika kipindi kimoja cha miezi 12 . Ufafanuzi huu pia huweza kutumika kwa dawa za kulevya zenye ishara ndogo au zisizoonekana za kimwili baada ya kuacha, kwa mfano, bangi.

Mwaka 2001, Chuo cha Marekani cha Dawa za Maumivu , Shirika la Maumivu Marekani na Shirika la Marekani la Dawa za kulevya, kwa pamoja zilitoa "Fafanuzi Zilizohusiana na Matumizi ya Opioidi kwa kutibu maumivu", ambayo ilibainisha zifuatazo masharti yafuatayo:

Matumizi ya vileo kimsingi, ni ugonjwa sugu, wa kinyurobiolojia, kutokana na sababu za jeni, kisaikolojia na hali za kimazingira zinazochangia ukuaji na kudhihirika kwake . Ina sifa za tabia ambazo ni pamoja na mojawapo au zaidi ya hizi: kuvurugika kwa udhibiti wa matumizi ya dawa, matumizi ya kuzoea, kuendelea kutumia licha ya madhara ya kutumia, na utashi mkubwa.

Utegemezi wa kimwili ni hali ya kujizoesha ambayo hudhihirishwa na dalili maalum za kuacha ambazo zinaweza kusababishwa na kuacha kighafla, kupunguza kiwango kwa kasi, upungufu wa kiwango cha dawa ya kulevya katika damu na/au utumiaji wa dawa kinzani.

Uzoevu ni hali ya mwili kujizoesha na dawa ya kulevya: kiasi kikubwa zaidi cha dawa ya kulevya zinahitajika jinsi muda unavyozidi ili kufikia matokeo kama ya awali jinsi mwili "anavyozoea kutumia" na kujizoesha matumizi hayo.

Utegemezi bandia wa dawa za kulevya ni istilahi ambayo imetumika kuelezea tabia za wagonjwa ambazo zinaweza kutokea wakati maumivu hayatibiwi vya kutosha. Wagonjwa walio na maumivu yasiyopunguzika wanaweza kulenga kupata dawa, "kwa muda fulani," ama wanaweza kuonekana vinginevyo kama 'wanaotafuta dawa' kwa njia isiyofaa." Hata tabia kama vile matumizi haramu ya dawa za kulevya na udanganyifu zinaweza kutokea katika juhudi za mgonjwa kupata nafuu. Utegemezi bandia wa dawa za kulevya unaweza kutofautishwa kutoka kwa utegemezi wa kweli kwa kuwa tabia hutoweka wakati maumivu yametibiwa kikamilifu.

Mwongozo wa Utambuzi na Takwimu za Matatizo ya Akili, DSM-IV-TR haitumii kamwe neno utegemezi wa dawa za kulevya. Badala yake ina sehemu kuhusu utegemeaji wa vileo

"Wakati mtu hushikilia matumizi ya pombe au dawa nyingine licha ya matatizo yanayohusiana na matumizi yake, utegemezi wa kileo inaweza kubainika. Matumizi ya kimazoea na matumizi ya mara kwa mara yanaweza kusababisha uzoelevu kwa athari za dawa ya kulevya na dalili za kuathithirika wakati matumizi yake yanapopunguzwa au kukomeshwa. Hii, pamoja na mabaya ya kileo huchukuliwa kama Matatizo ya Matumizi mabaya...."

Ufafanzi wa Utegemezi wa dawa za kulevya uliopendekezwa na Profesa Nils Bejerot:

"Hisia kwamivu (mtazamo) inayopatikana kwa kujifunza, ambayo hudhihirika wakati mwingine au daima kupitia tabia za kimaksudi, za kudhanika kwa mienendo na misukumo ya nguvu za asili, zinzzolenga uridhikaji maalum au kujiepusha na usumbufu fulani maalum".

 

Kwa hisani ya Mtandao

Ad