Ijue Benki kuu ya Tanzania
21 January 2016 | Benki Kuu
Benki Kuu ya Tanzania ni benki ya kitaifa inayosimamia masuala ya kibenki na kifedha. Makao yake makuu yapo Dar es Salaam nchini Tanzania. Kati ya majukumu yake ni utoaji wa fedha za Tanzania, Shilingi ya Tanzania.
Benki Kuu ya Tanzania iliundwa na Sheria ya Benki ya Tanzania 1965. Mwaka 1995, baada ya kuonekana kuwa benki hii ina majukumu mengi kuzidi uwezo wake, Sheria ya Benki ya Tanzania 1995 ilipitishwa na kuipa benki hii jukumu moja ambalo ni kusimamia sera ya fedha nchini.
Benki hii huongozwa na Bodi ya Wakurugenzi yenye wajumbe kumi.