Home » Afrika » Wafahamu mameya wawili wa Rwanda kutumikia kifungo cha maisha

Wafahamu mameya wawili wa Rwanda kutumikia kifungo cha maisha

05 July 2016 | Afrika

Wakili Mkuu wa Serikali nchini Rwanda jana siku ya jumatatu ameomba kifungo cha maisha jela dhidi ya mameya wawili wa zamani wa Rwanda, wanaotuhumiwa kushiriki katika mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi katika kijiji chao mashariki mwa Rwanda mwezi Aprili, 1994.

Baada ya miezi miwili kesi hiyo ikisikilzwa mbele ya Mahakama ya Paris, Philippe Courroye amewataja Octavien Ngenzi, mwenye umri wa miaka 58, na Tito Barahira, mwenye umri wa miaka 65, kama wahusika muhimu katika mauaji ya kimbari yaliyotokea katika wilaya yao ya Kabarondo, akimtaja Octavien Ngenzi kama "kiongozi" na tito Barahira kama mfadhili wa mapanga.

Ad