Uturuki haitaruhusu mpaka wa syria wa mjini Azaz kuangukia mikononi mwa wapiganaji
Uturuki imesema haitaruhusu mpaka wa syria wa mjini Azaz kuangukia mikononi mwa wapiganaji wa kikurdi wa nchini syria na kutoa onyo la makabiliano mara moja ikiwa watasonga mbele kukaribia eneo hilo.
Waziri mkuu wa uturuki Ahmet Davutoglu amekaririwa akizungumza hayo katika kituo cha televisheni cha NTV.
Uturuki imeshambulia ikiwalenga wapiganaji wa kikurdi wa syria tangu wikiendi huku ankara ikisisistiza ilikuwa ikijibu mashambulizi.
Ankara inawatuhumu wapiganaji wa YPG kuwa tawi la chama cha wafanyakazi wa Kikurdi PKK ambacho kimekuwa kikishambulia uturuki tangu miongo kadhaa iliyopita.
Jeshi la Uturuki limeendesha mashambulizi ya mabomu Jumapili hii kwa siku ya pili mfululizo dhidi ya ngome za wapiganaji wa Kikurdi, kaskazini mwa Syria, karibu na mji wa Syria wa Azaz katika jimbo la Aleppo.
Hali hii inatishia mpango wa kusitisha mapigano nchini syria, na kuingiliwa na hali ya sintofahamu, huku wahusika mbalimbali wa kimataifa, ikiwa ni pamoja Uturuki na Urusi, kutuhumiana kila mmoja kuchochea machafuko.