UNMISS, imeguswa na ripoti za matukio ya “ubakaji”
22 July 2016 | Afrika
Tume ya umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS, inasema imeguswa na ripoti za matukio ya “ubakaji”, yanayodaiwa kutekelezwa na wanajeshi wa Serikali na kwamba tuhuma hizo zimeanza kuchunguzwa.
Kwa mujibu wa UNMISS, inasema kuwa, idadi ya raia, wengi wakiwa ni wasichana wadogo, wamekuwa wakishambuliwa jirani na jumba la umoja wa Mataifa pamoja na maeneo mengine jirani kwenye jiji la Juba.
Hali hii imechangiwa na kuongezeka kwa machafuko kwenye maeneo mbalimbali ya nchi, toka kuzuka kwa mapigano majuma kadhaa yaliyopita, kati ya vikosi vya Serikali na vile vya waasi.